Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwegasira achaguliwa naibu meya Kinondoni

Achaguliwapic Data Rwegasira achaguliwa naibu meya Kinondoni

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Diwani wa Makongo, Joseph Rwegasira amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Kheri Missinga aliedumu kwa muda wa misimu mmoja.

Rwegasira ametangazwa kuchukua cheo hicho na katibu tawala wa wilaya ya Kinondoni, Stella Msofe baada ya kufanyika uchaguzi katika ukumbi unaotumika kuwakutanisha madiwani wote wa manispa ya Kinondoni.

Msofe ametangaza kuwa Rwegasira amefanikiwa kupata kura zote 25 kutoka kwa madiwani wa Kinondoni ambazo ni sawa na asilimia 100 pasipo hata moja kuharibuka.

Akizungumza jana Ijumaa Agosti 26, 2022 baada ya kuchaguliwa, Rwegasira amesema anashukuru kwa wale wote waliompigia kura na kumuamini kuwa anafaa katika nafasi ya naibu meya.

Pia, amesema angependa kumshukuru naibu meya alietangulia kabla yake kwani alifanya kazi kubwa wakati wa kipindi chake na mengi mazuri yanaonekana.

"Namshukuru naibu meya alietangulia, Kheri Missinga na ningependa kumuambia kuwa nitaendelea pale alipoishia" amesema.

Hata hivyo, amesema anamuahidi meya wa wilaya ya Kinondoni, Songoro Mnyonge kuwa ataifanya kazi yake kwa uadilifu na ufasaha wa hali ya juu.

Naye katika kuaga, Missinga amesema anapenda kuwashukuru waheshimiwa madiwani kwa kumuamini na kushirikiana nae katika kipindi chote cha uongozi wake kwani walimchagua kwa kishindo na anaamini alifanya mambo kama ipasavyo na anamtakia kila la kheri Naibu meya mpya.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz