Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwamlaza acharuka wabunge waliotimka Chadema kuitwa Covid-19

Rwamlaza Pic Rwamlaza acharuka wabunge waliotimka Chadema kuitwa Covid-19

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mbunge wa Viti Maalumu, Conschesta Rwamlaza amesema wanaowabeza wabunge 19 na kuwaita Covid-19 hasa wanapompongeza Rais Samia Suluhu Hassan, ni kwa sababu hawataki kukubali ukweli wa kazi yake.

Rwamlaza ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Aprili 17,2023 wakati akichangia kwenye hotuba ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Tamisemi kwa mwaka 2023/2024 ambapo amesema wabunge 19 wako kwa ajili ya kuwasimamia na kuwasaidia Watanzania.

Mbunge huyo amesema kwenye ukweli wataendelea kusema kuusema bila kuogopa kwasababu wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia.

Mbunge huyo ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema ambao wamekuwa kwenye mzozo na chama chao na tayari wamepelekana mahakamani wakidaiwa kuwa waliingia bungeni kinyume na sheria na utaratibu wa chama chao.

“Sisi wanatuita Covid-19, sawa lakini nataka kuwaambia kuwa ‘we are women at work’ (Wanawake tuko kazini) na kwamba tunakwenda na mama lakini kama kuna mwanaume atafanya kazi nzuri tutampongeza tu,” amesema Rwamlaza.

Mbunge huyo amemtaja Rais Samia kwamba aliwaita wanawake na kuwaambia kuhusu wanawake kushikamana kazi ambayo wataendelea kuifanya wakati wote.

Kauli ya mbunge huyo inakuja siku tatu baada ya mbunge wa Makambako, Deo Sanga alipomuomba Mbowe kuwasamehe wabunge hao ili waendelee kufanya kazi.

Sanga alitoa kauli hiyo Ijumaa Aprili 14, 2023 bungeni alipokuwa akichangia Hotuba ya Maombi ya Makadilio ya Fedha kwa Wizara ya Tamisemi ambapo alisema Mbowe anastahili pongezi kutokana na maridhiano aliyofanya na Rais Samia na kuomba pia Chadema kisisimamishe mgombea Urais 2025.

Chanzo: mwanachidigital