Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rungwe atetea nafasi yake Chaumma

50874 Pic+rungwe

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amefanikiwa kutetea nafasi hiyo baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Jumamosi Aprili 6, 2019 jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa uchaguzi, Mbwana Hassan Mbwana amesema Rungwe amepata kura za ndiyo za wajumbe wote 180 baada ya mpinzani wake, Issa Abbas Hussein kujitoa kwenye uchaguzi huo.

"Kwa matokeo haya, Rungwe atakiongoza chama chetu kwa miaka mingine mitano. Naomba tumpe ushirikiano hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani" amesema Mbwana.

Mwenyekiti huyo wa uchaguzi amewataja viongozi wengine waliochaguliwa kuwa ni Mohammed Masoud Rashid ambaye ametetea nafasi yake ya makamu mwenyekiti wa Chaumma - Zanzibar kwa kupata kura 176.

Amesema Kayombo Kaputari amepata kura 173 na kuwa mshindi wa nafasi ya makamu mwenyekiti wa Chaumma - Tanzania Bara.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Rungwe ameahidi kukipatia chama hicho ushindi katika chaguzi zijazo chini ya sera ya chama hicho ya uhakika wa chakula.

"Nitumie nafasi hii kuiomba Serikali itufungulie vyama vya siasa nasi tufanye mikutano ya hadhara ya kukijenga chama. Chaguzi ndiyo hizo zinakuja, tunahitaji kukutana na wanachama wetu," amesema Rungwe.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz