Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rita yaisajili bodi ya wadhamini upande wa Lipumba

45588 Pic+lipumba Rita yaisajili bodi ya wadhamini upande wa Lipumba

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bodi ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba imesajiliwa rasmi na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 8, 2019 amesema Rita imewaandikia barua inayoonyesha maombi yao ya kusajiliwa yamekubaliwa na bodi hiyo imesajiliwa.

Sakaya amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kurekebisha dosari walizoelezwa na Mahakama Kuu na hatimaye kukidhi vigezo vya kuwa na bodi inayotakiwa.

“Machi 6 nimepokea barua kutoka Rita ikionyesha maombi yetu ya kusajili bodi yamekubaliwa. Bodi yetu imesajiliwa na wajumbe wake wote nane,” amesema Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.

“Kinachofuata sasa tunasubiri bodi ikae ichague mwenyekiti wake na kuanza kufanya kazi ya kukiendesha chama ikiwemo kushughulikia kesi zilizopo mahakamani.”

Sakaya amegusia pia suala la chaguzi za ndani ya chama hicho na kueleza kuwa zitaendelea kama kawaida licha ya kesi zilizopo mahakamani.

“Hakuna sehemu inasema taasisi ikiwa na kesi haipaswi kuendelea na shughuli zake, Serikali ina kesi lakini inaendelea na utendaji kazi wake hata CUF iko hivyo,” amesema.

Soma zaidi: VIDEO: Prof Lipumba apata pigo la kwanza CUF



Chanzo: mwananchi.co.tz