Wed, 5 Apr 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ jana Aprili 4, 2023 ametoa wito bungeni jijini Dodoma kuwa iundwe tume maalum kwa ajili ya kuchunguza utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), akidai kwamba inalinda wabadhirifu wa fedha za umma.
“Haiwezekani tumejadili haya (ripoti CAG) mwaka jana na leo yanajirudia. Mtu anaiba huku, halafu nyie mnamhamisha mnampeleka halmashauri nyingine, huku anaendelea na uchunguzi na anatumia pesa zetu kugharamia kesi.
“Ngoma hii (ripoti ya CAG) ikija bungeni hatutaki tena kupiga swaga, ije tulale nao mbele" amesema Musukuma.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live