Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kuongoza kamati kuu CCM

Samiaa Pic Ccm Rais Samia kuongoza kamati kuu CCM

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano, Septemba 7, 2022 anaongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.

Katika kikao hicho kinafanyikia Ofisi ndogo za chama, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kujadili masuala mbalimbali, kitajadili na kupitia majina ya wanachama walioomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala)

Tayari mchujo wa wagombea ulifanyika Septemba 4 na 5, 2022 makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Jana Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa ya uchaguzi huo wa wajumbe tisa utakaofanyika Septemba 22, 2022 saa 5:00 asubuhi, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.

Hadi sasa vyama vya ACT-Wazalendo na CUF wameshakamilisha mchakato wa kupata majina ya watakaoenda kupigiwa kura Bungeni huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kutoshiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live