Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia atoa Sh5 milioni kumuenzi Chifu Mkwawa

Mkwawa Pic Rais Samia atoa Sh5 milioni kumuenzi Chifu Mkwawa

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu ametoa Sh5 Milioni 5 kama mchango wake kwa ajili ya kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Chifu Mkwawa katika eneo la Kalenga, Jimbo la Kalenga mkoani Iringa.

Maadhisho ya kumbukumbu ya miaka 120 ya kifo cha Chifu Mkwawa yanatarajia kufanyika kwa siku kadhaa yakianza Juni 17, 2023 katika eneo la makumbusho ya Mkwawa la Kalenga.

Akikabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa,  Daud Yassin  amesema Rais Samia ambaye ni  Mwenyekiti wa CCM Taifa anatambua na  kuthamini juhudi zilizofanywa na machifu hapa nchini akiwemo Chifu Mkwawa.

Amesema kwa sababu anatambua umuhimu wa maadhimisho hayo ametoa mchango wake wa fedha kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema kila mwaka wataendelea kufanya maadhimisho hayo na kulifanya eneo hilo liendelee kuwa la utalii likikusanya wageni wengi.

Amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano na kuachana na mambo yote yasiyo na tija.

"Sisi sote ni ndugu, tuivae siku hii kuanzia ngazi ya familia tukidumisha amani, mshikamano na upendo. Tusibaguane," amesema Dendego.

Awali Chifu wa Wahehe, Adam (II) Mkwawa aliwashukuru Watanzania kwa kuendelea kukumbuka jitihada za Mkwawa katika harakari zake za ukombozi.

Baadhi ya wakazi wa Kalenga wamesema wanatamani kuona Makumbusho ya Mkwawa yanaendelea kuenziwa na kufanywa kuwa kituo cha utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live