Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia atoa Mil. 200 kujenga zahanati Mirerani

Rais Samia Korea . Rais Samia atoa Mil. 200 kujenga zahanati Mirerani

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC - Itikadi , Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla akizungumza na wana Mirerani amesema najua mnashida kule mgodini moja nimekuja na Naibu Waziri wa Madini Mhe Kiruswa atamaliza hapahapa nyingine ni suala la kupata zahanati nami naimaliza hapahapa nampigia Waziri mhusika wa Wizara ya Tamisemi amalize kabisa suala hili .

Nae Waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Mchengerwa akijibu kwa njia ya simu amesema

“Kama Waziri wa Nchi ninaewakilisha Ofisi ya Rais nimesema dhamira yetu ni dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona Watanzania wanapata Huduma bora za Afya wakiwa karibu na maeneo kama ni maeneo ama maeneo ya Makazi kwahiyo hoja hii umenieleza leo mimi kwakua Mkurugenzi ameshaanza taratibu kwa kushirikiana na wadau na sisi Ofisi ya Rais Tamisemi kuwaahidi Wananchi wa eneo kwanza nawaelekeza Wataalamu wangu kwanza watakuja kuona halisi”

“Pili namuelekeza Katibu Mkuu aweze kutenga fedha pamoja na kwamba wadau watatuchangia na sisi ambao tunawajibu wa kusimamia Afya ya msingi tutatoa fedha Shilingi Milioni 200 itatosheleza kabisa kuanza kujenga Majengo ambayo yatatosha kabisa kuanza huduma kama Kituo cha Afya.”

Kisha akaahidi kuwa atafika katika eneo hilo kwa ajili ya kutembelea na kuangalia Utekelezaji wa Mradi huo pindi utakapoanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live