Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aongoza kikao cha CCM, kuchukua hatua wanaovunja maadili ya chama

WhatsApp Image 2021 07 29 At 11.11.34 PM 660x400.jpeg Rais Samia aongoza kikao cha CCM, kuchukua hatua wanaovunja maadili ya chama

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo July 29, 2021 ameoongoza kikao maalum cha kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichokutana Ikulu Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine kamati Kuu imempongeza Rais Samia kwa uamuzi wa kuruhusu chanjo ya virusi vya Ugonjwa wa Corona (Uviko 19) kutolewa nchini na yeye kuwa mfano wa kukubali kuchanjwa ikiwa ni  udhibitsho wa usalam wa chanjo hiyo.

.

Uamuzi wake umetajwa kuwa ni kielelezo cha upendo na uzalendo mkubwa alionao katika kujali Afya za watanzania na ni hatua nzuri ya Tanzania kuungana na dunia katika kukabiliana dhidi ya UVIKO-19, pia ikiwa sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020- 2025 ibara ya 83 na namba 84.



.

Kamati Kuu imeeleza kuanza kuchukua hatua kwa wala wote wanaokiuka mienendo , taratibu na kanuni za maadili na uongozi kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Mapinduzi.



.

RAIS SAMIA KUPOKEA NDEGE MPYA, ATCL WAFUNGUKA “HII ITAKUWA YA TISA”
Chanzo: millardayo.com