Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Rais Samia ana uwezo mkubwa wa uongozi’

6c33abd5c6492ecf333a5f36a575695d.jpeg ‘Rais Samia ana uwezo mkubwa wa uongozi’

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Erick Ambakisye amesema Rais Samia Suluhu Hassan ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi zake na kusimamia miradi mbalimbali aliyoacha Rais John Magufuli.

Amesema katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli, Watanzania wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kuendelee kuiombea serikali iweze kutekeleza vizuri Ilani ya CCM na kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

“Namtazama Samia kama Rais mwenye uwezo wa kufanya kazi nzuri na kubwa sana. Tumeona alikuwa akifanya kazi nzuri sana akiwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,” alisema Ambakisye.

Alisema Watanzania wanapaswa kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili watimize kauli mbiu ya 'Hapa Kazi' iliyoachwa na Magufuli, pamoja na kushirikiana vyema na viongozi wa serikali.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza (MPC), Erick Soko alisema ana imani kubwa na Rais Samia.

“Mama Samia atasimamia miradi vyema kwani miaka mitano alikuwa msaidizi wa Rais Magufuli hivyo mambo mengi anayajua vizuri. Uzuri wa miradi mingi ya kimkakati tayari mipango yake ipo na Mama Samia atakuwa na jukumu la kuisimamia tu,” alisema Soko.

Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa, Askofu Charles Sekelwa alisema chini ya Rais Samia, miradi itakamilika kwa wakati na kodi itakusanywa na kwamba anawaombea kwa Mungu viongozi wote wapewe hekima na busara.

Mchungaji wa Kanisa la ACT, Abel Lugaila aliwataka Watanzania waendelee kuiombea serikali na Rais Samia na wasaidizi wake ili Tanzania iendelee kupaa kwa maendeleo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz