Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia akutana na Jesca Magufuli, atoa maagizo haya

Samia Jesika Magufuli.jpeg Rais Samia akutana na Jesca Magufuli, atoa maagizo haya

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Jesca Magufuli, mtoto wa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli mara baada ya kuhutubia vijana wa UVCCM baada ya kupokea matembezi ya vijana wa chama hicho, ikiwa ni shamrashamra za kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika kwenye Viwanja vya Maisara, Zanzibar, leo Jumatano Januari 10, 2024.

Katika hotuba yake, Rais Samia amepongeza matembezi hayo kwani yameonyesha utayari wa vijana kwa kujikumbusha, kuyalinda na kuenzi mapinduzi matukufu yaliyoondosha ubaguzi kisiwani humo.

"Nina imani na vijana kila ninapokutana nanyi, ila mnapaswa kubadilika na kufanya mambo mazuri ikiwamo kujibidiisha kwenye masomo yenu na kuongeza maarifa zaidi ili kupambana na mabadiliko yaliyopo," amesema Samia.

Rais Samia amesema,"Nina kauli yangu kila siku nasema tusiende kulumbana, twende tukajenge hoja, naamini UVCCM inao vijana wa kulitekeleza hilo, msikubali dhana potofu ya kusubiri vyeo, umoja huu upo katika kuilinda na kutetea nchi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live