Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Ruzuku kwa vigezo, sio kwa wote

Vyama Vya Siasa Ruzuku Kizungumkuti Ruzuku vyama vya siasa kipo palepale

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia kuwepo kwa maoni mengi kuhusu utolewaji wa ruzuku ili kunusuru vyama vya siasa ambavyo vingi vipo hatarini kupotea kufuatia kukosa fedha za kujiendesha, Rais Samia amesema kuwa Serikali haina fedha kufadhili uendeshaji wa vyama hivyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa leo Machi, 21, 2022 Ikulu ya Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa hata akikubali kutoa fedha hizo bado hana pakuzitoa kwa sasa.

Amesema kuwa sio rahisi kwa Serikali kuendesha vyama vyote vya siasa kwani haiwezekani kuanzisha chama ka kutegemea fedha za serikali ili kujiendesha.

"Hata nikisema ndio kwenye maombi hayo ya ruzuku, fedha hizo nitazitoa wapi? sina pa kuzitoa naomba hili tukaumize vichwa wote"

"Hivi vyama vinavyojiendesha vinawezza vipi kujiendesha?"

"Na unaposema sawa kwenye hili tutakuwa kama Lesotho, kila mara baada ya siku mbili chama cha siasa kinasajiliwa wanataka ruzuku haipo hivyo"

"Unapoanzisha chama cha siasa ni cha kwenu huwezi kutegemea Serikali ikuendeshee chama chako"

"Ruzuku zipo kwa vyama vilivyo na uwakilishi bungeni vinavyopiga kazi" Amesema Rais Samia"

Ameongeza kusema kuwa " Ruzuku kwa vigezo sio kwa wote"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live