Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Gwaji Boy utachanja huchanjii?

17bdd48d5e5d08775fa236032370d9d4 Rais Samia: Gwaji Boy utachanja huchanjii?

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Samia Suluhu amemuhoji Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kuwa atachanja chanjo ya Corona au hachanji?

Rais Samia amemuhoji Gwajima leo katika mkutano wake wa adhara na wananchi, Tegeta jijini Dar es Salaam alipokuwa akielekea Bagamoyo.

Rais Samia akimkaribisha Gwajima kuzungumza alihoji “Gwaji Boy oyeee, mtachaja au hamchanji?

Wananchi: “Tunachanjaaaaa.........

Hata hivyo, Gwajima alipokaribishwa kuzungumza na wananchi alijielekeza kuzungumzia changamoto za jimbo hilo na kukwepa kujibu swali alilouliza Rais hasa ikizingatiwa Mbunge huyo ameweka wazi msimamo wake wa kutochanja chanjo ya corona.

Gwajima alimshukuru Rais Samia kwa fedha zilizoelekezwa katika jimbo hilo kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema wana Kawe si kwamba wanampenda Rais Samia pekee bali ni rafiki kwa kuwa amewafanyia makubwa jimbo hilo.

“Mama Samia ni rafiki yetu, aliwahi kufungua ofisi kule Mabwepande wakati akiwa makamu wa rais, lakini alipoingia madarakani kama Rais ametupendelea wana Kawe.

“Ametupatia bilioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa barabara 114 kupitia Tarura, lakini kuanzia Septemba 10 maji kutoka Ruvu chini yataanza kusambazwa kupitia matenki yaliyojengwa,” alisema.

Alisema mbali na hayo, jimbo hilo linakabiliwa na uhaba wa shule hususani katika mtaa wa Wazo.

“Kule hakuna shule kabisa kuanzia msingi na sekondari… watoto wanakwenda kusoma Kunduchi na kuhatarisha maisha yao kwani wanagongwa na magari.

“Pia kuna suala la mafuriko, ulipokuwa ukigombea mwaka jana uliahidi sh bilioni 5 za kumaliza tatizo la mafuriko katika eneo la Chasimba, watu wengi wamepoteza maisha katika eneo hili, hivyo tunakukumbusha mama,” amesema Gwajima.

Chanzo: www.habarileo.co.tz