Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Amlilia Mwenyekiti wa CCM Kusini Unguja

Samia 2 7?fit=700%2C468&ssl=1 Rais Samia Amlilia Mwenyekiti wa CCM Kusini Unguja

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rais Samia Amlilia Mwenyekiti wa CCM Kusini Unguja July 27, 2021 by Global Publishers



Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdallah Ali au maarufu kama Mzee Kichupa, aliyefariki leo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja visiwani Zanzibar.

Katika salamu hizo, Rais Samia amesema CCM imempoteza kiongozi mzalendo, mwenye msimamo thabiti na muumini wa kweli wa muungano, mapinduzi na siasa za utaifa na kwamba marehemu alikuwa mwalimu, mwelekezi na mshauri mzuri wa masuala ya uongozi, uzalendo, utaifa na masuala yote ya siasa.

Enzi za uhai wake, marehemu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama tangu enzi za ASP hadi CCM, zikiwemo Katibu Mkuu wa CCM wilaya na mkoa, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mbunge na baadaye kuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, nafasi ambayo amedumu nayo hadi alipofikwa na mauti.



Share this:TweetWhatsApp Related
Chanzo: globalpublishers.co.tz