Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli aelezea rekodi uchukuaji fomu Ubunge

A6c2aaca33f67d60ecbd48aedf8241ab Magufuli

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS Dk John Pombe Magufuli amewapongeza waliochukua fomu za kugombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba idadi kubwa ya waliojitokeza haijawahi kutokea kwenye chama hicho.

Akizungumza baada ya uapisho wa Viongozi walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali Ikulu ya Chamwino, Dodoma leo, Rais magufuli alisema,"Waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge kupitia CCM Tanzania nzima wamefikia 10,367 na katika hao ambao wamekamilisha taratibu zote na kurudisha fomu zao zikiwa kamili ni 10,321 na ambao hawakuzirudisha ni 46 tu nchi nzima...

"...kiukweli wengi sana wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge kupitia CCM. Wamefikia 10,367 haijawahi kutokea kwamba katika chama kimoja wagombea kitu cha ubunge pekee wanafikia idadi hii. Bado udiwani, nawapongeza sana waliochukua fomu," alisema Rais Magufuli.

Chanzo: habarileo.co.tz