Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli achukua Fomu kugombea Urais awamu ya pili

1596653584 Presidentmagufuli052020 1588668248?fit=800%2C420 Rais Magufuli achukua Fomu kugombea Urais awamu ya pili

Thu, 6 Aug 2020 Chanzo: dar24.com

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Magufuli, leo 06 Agosti, 2020 amechukua fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma.

Zoezi hilo ambalo limeongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijageikiwa ni utekelezaji matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais Magufuli amechukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha Pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

Na mara baada ya kuchukua fomu, Rais Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu.

Chanzo: dar24.com