Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla aibuka sakata la Dk Bashiru

RC Makallaa RC Makalla aibuka sakata la Dk Bashiru

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally akiendekea kuandamwa na kauli yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amejitosa akimtaka kiongozi huyo kukaa kimya kama hataki kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kauli ya Bashiru inayoonekana kuzua utata ndani ya chama hicho ilitolewa siku za hivi karibuni wakati akihutubia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) uliofanyika mkoani Morogoro, alipowataka kuacha kusifia kila jambo huku wakijua wanachangamoto zinazowakabili.

Makalla akizungumza jana Ijumaa Novemba 25, 2022 wakati anapongeza juhudi za Rais Samia katoa fedha Kwa ajili ya miradi ya maji, baada ya kiongozi huyo kutembelea chanzo cha Maji Ruvu Juu. Amesema Watanzania bado wanaendelea kumshukuru Rais kwa Juhudi anazofanya na watu wenye kelele kama Dk Bashiru ni bora wakae kimya.

"Sisi bado tutaendelea kushukuru jitihada za Rais Samia kama ilivyo utamaduni wetu lakini hizo kelekele hizo zakina Dk Bashiru Ally mi nasema ni kilanga Sisi tunasema tuko saiti akate Simu, tupo saiti tutaendelea kushukuru kwakuwa ni utamaduni wetu,

"Na tunajua mradi mkubwa wa kidunda ambao ni tumaini letu unakuja tutaendelea kushuru Juhudi za Rais kuwaletea watanzania maendeleo, kama yeye ananyongo yake ya chuki aache akale ndimu ili kuondoa radha ya nyongo lakini akumbuke sisi tuko saiti tunashukuru ndiyo maana kuna maneno hata ya kiingereza thank you!," amesema

"Kwahiyo mtu asiye taka kama Bashiru akale ndimu na sukari lakini sisi atuache tuko saiti tunaendelea kufanya kazi na kutangaza mazuri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan," amesema

Chanzo: Mwananchi