Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Muhongo achangia ujenzi maktaba Shule ya Karubugu

9160171903cd1e3d299414a016dcdf6b Profesa Muhongo achangia ujenzi maktaba Shule ya Karubugu

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo jana amechangia mifuko ya saruji 50 kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa maktaba linalojengwa katika Shule ya Msingi Karubugu iliyopo jimboni humo mkoani Mara.

Katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, wananchi wa jimbo hilo wanaendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia katika shule za msingi na sekondari zilizopo jimboni humo ikiwemo ya Karubugu.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Ramadhan amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 830 na walimu watano ambapo imekuwa ikifanya vizuri katika kufaulisha wanafunzi. Mwaka 2020 shule hiyo ilifaulisha wanafunzi wote 82 waliofanya mtihani wa darasa la nne na kufaulisha 60 kati ya 73 wa darasa la saba.

Mtendaji wa Kijiji cha Kurwaki, Abeid Makamba Ndagala amesema ujenzi wa maktaba hiyo ya kisasa ulianza wiki mbili zilizopita ambapo wanatarajia kukamilisha ujenzi huo mwisho wa mwezi huu.

Washiriki wakubwa wa ujenzi huo ni wanakijiji wa jimbo hilo ambao wamekuwa wakichangia Sh 5,000 kwa kila nyumba, wengine wakitumia nguvu kazi kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji katika kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz