Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Maghembe awapa somo Hai

17426 MAGHE+PIC TanzaniaWeb

Sun, 16 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Wananchi wa Kata ya Machame Uroki mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuwaepuka wagombea ambao hawawezi kuwaletea maendeleo na kuhakikisha wanawachagua wale wanaolenga maendeleo ya wananchi.

Rai hiyo ilitolewa juzi na mbunge wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe wakati akimuombea kura mgombea wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM, Robson Kimaro.

Maghembe alisema huu si wakati wa kuhangaika na wagombea ambao wanahangaika kwa ajili ya matumbo yao na kwamba ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanawachagua viongozi ambao watawaletea maendeleo ya kweli.

“Ndugu wananchi, achaneni na watu ambao hawawezi kuwaletea maendeleo, chagueni mtu ambaye analenga maendeleo ya watu na ambaye atasimama kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Maghembe.

Maghembe aliwaomba wananchi kumchagua mgombea wa CCM ili kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa huduma ya umeme pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara.

“Mkitupa diwani wa CCM, tutaboresha miundombinu ya barabara, umeme, shule na kupanua zahanati yenu, ambayo imekuwa kilio kikubwa kwenu, mkiomba ipanuliwe na kupandishwa hadhi kuwa kituo cha afya,” alisema.

Akiomba kura, Kimaro aliwaomba wananchi wa kata hiyo msamaha kwa maamuzi aliyochukua ya kujiuzulu na kueleza kuwa alifanya hivyo kwa nia njema ya kuhakikisha anawaletea maendeleo.

Chanzo: mwananchi.co.tz