Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Lipumba awashukia wapinzani wanaohamia CCM

17537 LIPUMBA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa vyama vyaSsiasa, Profesa Ibrahim Lipumba amewashukia wapinzani wanaohamia CCM wakidai kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Amesema Rais Magufuli anaweza kuungwa mkono bila mhusika kuhamia CCM.

Akizungumza leo Jumamosi Septemba 15, 2018 katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa chama hicho jimbo la Ukonga, Profesa Lipumba amesema mgombea ubunge wa  CCM Ukonga, Mwita Waitara amewasaliti wananchi si Chadema pekee.

Waitara alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema kuanzia mwaka 2015 hadi Julai 28, 2018 alipojiuzulu na kujiunga na CCM, kupitishwa kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

 “Waitara akumbuke kuwa alichaguliwa na watu wa vyama vyote siyo Chadema pekee, lakini leo hii amewasaliti na kuhamia CCM, anakuja kuomba kitu gani kwenu?”amehoji.

“Kama umeamua kuunga mkono juhudi za Rais unga ukiwa kwenye chama chako, iweje uwakimbie wananchi wako, iweje ujiuzulu ubunge?”

Amesema hakuna alichokifanya Waitara mpaka sasa kwani hali ni mbaya katika jimbo hilo.

“Mtu anahama chama anasema anaunga mkono mazuri yanayofanyika CCM,  kwa mazuri gani, wakati vijana njaa imepanda kichwani?  Hali inakuwa ngumu kwa sababu ya sera, ili nchi ipate mafanikio inatakiwa itoe mikopo kutoka sekta binafsi,” amesema.

Amesema kutokana na sera mbovu, kwa sasa mfumo wa biashara haujakaa vizuri, biashara hazitoki na hakuna mzunguko wa fedha.

Amewataka wakazi wa Ukonga kumchagua mgombea ubunge wa CUF, Salama Masoud akadai haki na demokrasia.

Chanzo: mwananchi.co.tz