Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Lipumba auzungumzia mgogoro uliokuwa CUF

78580 Pic+lipumba

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simiyu. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema mgogoro uliokuwepo ndani ya chama hicho uliwapotezea muda.

Hayo yalisemwa jana Ijumaa Oktoba 5, 2019 katika kongamano la sauti ya haki na furaha kwa wote lililofanyika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu na lililoongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba alisema katika mgogoro huo walibaini aliyekuwa akiwachelewesha huku akisema pamoja na kupotezea muda bado haujamalizika wanayo nafasi ya kujipanga na kusonga mbele.

"CCM imekuwa sio chama cha siasa kimekuwa chama dola sisi tukiwa tunaita viongozi wetu kwaajili yakupanga mikakati wao wamekuwa wakiita watendaji," alisema Profesa Lipumba

Alisema kama wananchi wakiamua CCM hawawezi kuzuia mabadiliko kwa kutumia vyombo vya dola.

Awali, aliyewahi kuwa mbunge wa Maswa (Chadema) kabla ya kuhamia CUF, Silvester Kasulumbai alisema watajipanga kuanzisha kanda ya ziwa  kati ya blue na nyekundu.

Pia Soma

Advertisement
Alisema rangi ya blue itasimamia watu watekeleze haki za binadamu dhidi ya uonevu unaofanyika pamoja na maandalizi yanayofanywa ya kuiweka Tanzania ya kijani.

"Mikoa hii itaepukana na uonevu kwa sababu itakuwa na watu wanaojali haki za binadamu na kuepuka uonevu na ukandamizaji," alisema

Alisema demokrasia sio kitu cha mtu mikoa hiyo itakapojengwa kwenye rangi nyekundu na blue hata hali ya kuzuia demokrasia na kutisha haitakuwepo kila mmoja atakuwa anajitambua.

CUF kikiongozwa na Profesa Lipumba kinaendelea na ziara katika mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz