Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Lipumba asema CUF kitashiriki uchaguzi wa Jang’ombe

12284 LIPUMBA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza kuwa chama hicho kitashiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang'ombe utakaofanyika Desemba mwaka huu.

Lipumba ametoa kauli hiyo leo Agosti 16 katika mkutano na waandishi na habari huko Malindi Mjini Unguja, wenye lengo la kutoa msimamo wa chama chake juu ya ushiriki wao katika chaguzi ndogo ndogo za wabunge na wawakilishi.

Amesema kwa kuwa CUF ni sehemu ya vyama vya siasa ambavyo vina haki ya kushiriki uchaguzi huo wa marejeo hivyo ni wazi kuwa hawataacha kushiriki uchaguzi ili kuwapa fursa wananchi kukichagua chao hicho ili kuwatumikia .

Amesema uongozi wa chama chao hivi sasa upo katika michakato ya kumpata mgombea atakaye peperusha bendera ya kuwania uwakilishi kupitia Chama chao cha CUF.

"Hatuwezi kuwaachia fursa ya kushiriki uchaguzi mdogo kwa kisingizio cha mgongano uliopo baina yetu, sisi lengo letu ni kutumikia wananchi hivyo tunaahidi kuwa tutashiriki uchaguzi bila ya wasi wasi wowote,"amesema Lipumba.

Ameongeza kuwa;

 "Kutoshiriki uchaguzi ni sawa na kuwasusia wananchi wetu hivyo kwa upande wetu sisi hatuwezi kuwasusia wananchi hata kidogo, bali nguvu zaidi tutazitoa ili kuhakikisha tunafanya vyema katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi,"

Hata hivyo Lipumba alimtaka Maalim Seif Sharif Hamad kufuta kesi zisizo na mashiko walizofungua mahakamani ili kuepukana na hasara ambazo zinaweza kuepukika

Amesema si jambo la busara hata kidogo kwa wakati huu ambao nchi ipo katika kipindi kizuri cha amani na utulivu huku kundi la watu likaibuka na kuanza kufungua kesi za kisiasa ambazo kuwepo kwake ni kupoteza muda kwa kundi lililofungua kesi hizo.

"Niwaombe sana ndugu zangu akina Maalim Seif kufuta kesi zao

Mahakamani kwani kinyume chake wataendelea kuwanufaisha mawakili tu wala hakutakuwa na jambo jipya juu ya kesi hizo"alisema Lipumba.

Akizungumzia kuhusiana na mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika hivi karibu amesema kuwa viongozi wapo katika mipango ya kuandaa mkutano huo ambao utakuwa ni fursa pekee kwa wanachama kuwania nafasi ya uongozi wanayoitaka.

"Kwa kuwa chama chetu kipo kwa ajili ya kutumikia wananchi ndio maana hivi sasa tumo katika maandalizi ya kufanya mkutano mkuu ambao utatoa viongozi wapya wa kukitumika chama hicho bila ya ubaguzi,"amesema Lipumba.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz