Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Lipumba aeleza alivyojiweka kando na Lowassa 2015

Video Archive
Tue, 17 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameweka wazi kuwa alijiweka mbali na siasa mwaka 2015 kwa kuwa hakutaka kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa.

Profesa Lipumba amesema hilo limetokana na nafsi yake kutokubali kumnadi mtu atakayepambana na ufisadi wakati na yeye ana tuhuma za ufisadi.

Ameyasema hayo leo Jumatatu, Machi 16, 2020 katika mahojiano maalum aliyofanya baada ya kutembelea ofisi za Mwananchi. “Dk Slaa(Wilbroad) alitaja orodha ya mafisadi ikiongozwa na Edward Lowassa, na mfano ikaonekana kwenye mradi mmoja huko Monduli,” “Sasa leo hii nipite nchi nzima kumnadi kuwa atakuwa kamanda wa kupambana na ufisadi, hapana kwa kweli hata kama mzigo mzito mpe mnyamwezi ila mnyamwezi mie huu mzigo umenishinda,” amesema Profesa Lipumba

Amesema akaona ni vyema akae pembeni kupisha uchaguzi upite na yeye akaamua kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida.

Chanzo: mwananchi.co.tz