Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Kitila: Siasa isipompa mtu hela ni hatari sana

Kitila Pc Data Profesa Kitila: Siasa isipompa mtu hela ni hatari sana

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo amesema anachukulia kwa uzito hali ya ugumu wa maisha inayowakabili Watanzania, akisema kama siasa haitatibu matumbo itakuwa hatari.

Profesa Mkumbo ameeleza hayo jana Jumapili Oktoba 16, 2022 wakati akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Manzese.

“Kama siasa ikifanyika halafu mtu hana hela ni hatari sana, kama mbunge nalichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa sana,” amesema Profesa Mkumbo.

Kwa upande wa Serikali hali hii inasababishwa na hali ya hewa, ikiwemo ukame na vita vya Russia na Ukrine, lakini imejitahidi kuppunguza ukali wa maisha kwa kuweka ruzuku kwenye mafuta kila mwezi.

“Mimi kama mbunge nitaendelea kusimamia kuhakikisha sera za kikodi, hazimuumizi mwananchi,” amesema.

Aidha Profesa Mkumbo amewashauri wananchi kutunza vyakula pamoja na kutumia maji kwa uangalifu, kwani hali ya hewa ikiendelea hivi kuna uwezekano wa kuwa na ukame.

Kuhusu matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo amesema, fedha hizo sio siri, kama mbunge ameamua kuweka wazi matumizi yake kwa kuunda kamati.

“Nimeunda kamati ya mfuko wa jimbo, inayohusisha madiwani wote na watendaji wa taasisi za kiraia ili kuangalia ni wapi penye changamoto zaidi papewe kipaumbele,” amesema na kuongeza.

Chanzo: mwanachidigital