Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof. Muhongo kuwafikia wananchi kwa urahisi

8c33bef406b0e565781bb2f9d21aa758 Prof. Muhongo kuwafikia wananchi kwa urahisi

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof Sospiter Muhongo ameanzisha utaratibu wa kupita nyumba hadi nyumba na maneno ya kazi ili kusikikiza kero za wananchi wa jimbo la musoma vijijini mkoani mara.

Katika kutekeleza adhma hiyo, Prof Muhongo aligawa pikipiki sita kwa wasaidizi wake ili ziwasaidie kutekeleza mpango huo kwa urahisi.

Muhongo aliwapangia wasaidizi wake maeneo ya kazi ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na kuwataka kukabidhi ripoti zao kila jumamosi kwa mbunge huyo.

Aidha, ameToa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na simu janja ‘Smartphone’ sambamba na vifurushi vya internet, Kompyuta mpakato ‘Laptop’ na vifaa vinavyopima na kutambua eneo ‘GPS.

Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374.

Chanzo: www.habarileo.co.tz