Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof. Lipumba awaomba radhi Wazanzibar, yupo tayari kuachia Uenyekiti wa CUF

Lipumbaaapic Data Prof Ibrahim Lipumba aomba radhi

Sat, 12 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, leo Jumamosi tarehe 12 Februari, 2022 amesema nafasi yake iko wazi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza leo Februari 12, 2022 akiwa anazungumza na vyombo vya habari, amabao amesema kauli anaitoa kufuatia kuwafanya Wanachama wa Chama hicho kufahamu kuwa nafasi hiyo hipo wazi kwa yoyote anayetaka kugombea.

Pia Prof. Ibrahim Lipumba amewaomba radhi watu wote waliokwazika kwenye mgogoro uliojitokeza baina yake na Maalim Seif Shariff ambaye alikuwa katibu Mkuu wa Chama hicho kufuatia Lipumba pamoja na wenzake tisa kufukuzwa, kabla ya kutambuliwa na Ofsi ya Msajili wa Vyama vya siasa kuwa ni Mwenyekiti halali wa Chama hicho.

"Natoa wito na kuwahakikishia wanachama kwamba, hii nafasi ya mwenyekiti iko wazi kwenye uchaguzi unaokuja, kwa maana kwamba kila mmoja anaweza kugombea nafasi hiyo.

“Nawaomba radhi Wazanzibar niliowakwaza katika mgogoro, nawakaribisha tujenge chama. Kwa upande wangu wakati wa mgogoro hawakunitendea haki na kunielezea mambo yasiyo ya kweli niliyoyasikia na nisiyoyasikia, nimewasemehe yaliyopita si ndwele.

“Nasisitiza vijana tujitokeze kugombea nafasi zote ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa Taifa, kwamba Lipumba hajawa na hatakuwa kikwazo kwa watu kujitokeza kugombea nafasi hizo,”- Lipumba.

Kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikiandamwa na migogoro isiyokwisha kitendo kilicho pelekea aliyekua katibu mkuu wa chama, Hayati Maalim Seif Shariff Hamad kuhamia chama cha ACT Wazalendo.

Hatua ya Prof.Lipumba kutangaza utayari wake wa kuachia nafasi hiyo inatajwa kua ni dalili ya kuwavuta wanachama waliokimbia chama hiko ambao siku chache zilizopita walitangaza kujiondoa ACT Wazalendo.

Prof. Lipumba amewataka wanachama wa chama hicho watakao kuwa tayari kuwania nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2022 kujitokeza kwenye kinyanganyiro

Chanzo: www.tanzaniaweb.live