Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof. Lipumba afunguka kuhusu hali ya demokrasia na utawala wa Rais Samia

Picchaossupremeaslipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Rais Samia Suluhu Hassan akisimamia masuala ya utawala bora, kujenga demokrasia na uchumi shirikishi ataingia kwenye rekodi n ahata kupata tuzo ya Mo Ibrahim.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo Agosti 19 jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Amesema akipata nafasi ya kukutana na Rais Samia atamshauri asimamie masuala ya utawala bora, demokrasia na uchumi shirikishi na kwa kufanya hivyo atajijengea heshima kubwa.

“Natarajia nikipata fursa ya kukutana naye nitamwambia ajiwekee malengo kwamba, akimaliza muda wake apate tuzo ya Mo Ibrahim kwa kusimamia utawala bora, kujenga demokrasia na kujenga uchumi shirikishi,” alisema Profesa Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa Cuf amesema Rais Samia alipoapishwa Machi 19,2021 alianza kuvutiwa na hotuba zake alizokuwa akizitoa mwanzoni lakini, baadaye anaona mambo yamebadilika na ana shaka siku za usoni mambo yatakuwaje.

Hata hivyo, amesema licha ya shaka yake lakini hajapoteza matumaini kwa sababu Rais Samia bado anayo nafasi ya kufanya mabadiliko katika taifa endapo ataamua kusimamia utawala bora, kujenga demokrasia na kujenga uchumi shirikishi.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz