Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof Kabudi amfagilia Rais Samia Bungeni

Dmzaz FXoAEsM58 (1) Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Kilosa.

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa jimbo la Kilosa, Prof Palamagamba Kabudi, amemfagilia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali jimboni kwake.

Kabudi amezungumza hayo leo Juni 20, 2022 alipokuwa akitoa mchango wake wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2022-23 bungeni jijini Dodoma.

Amesema anamshukuru Rais Samia kwani kwenye jimbo lake, fedha nyingi zimetolewa katika sekta afya, elimu, maji, barabara, madaraja na kilimo cha umwagiliaji.

"Kwenye elimu tumepewa jumla ya Bil. 2.3 ujenzi wa shule ya sekondari ya Berega na shule ya Kata ya Maguha, tumepewa Sh bil 2.4 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati na pia ametoa Mil. 900 kwa ajili ya kituo cha afya katika milima ya Uponela," alisema Kabudi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live