Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wazuia mkutano wa ‘CUF Lipumba’

46230 Cufpic Polisi wazuia mkutano wa ‘CUF Lipumba’

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkutano uliotakiwa kuanza leo Jumanne Machi 12, 2019 wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Profesa Ibrahim Lipumba umezuiwa.

Taarifa ya kuzuiwa huko imeletwa katika eneo la mkutano huo Hoteli ya Lekam Buguruni na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam. "Tumekuja kuwaeleza kuhusu zuio hili kwa sababu wameshalipeleka makao makuu ya Polisi," amesema Chembera.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, Thomas Malima na Naibu Katibu mkuu (Bara) Magdalena Sakaya wamesema hawajapata katazo hilo kwa hiyo wataendelea na mkutano. "Sisi hatujapata hilo katazo, tunaendelea na mkutano," amesema Malima.

Awali, akizungumzia na waandishi wa habari, mkurugenzi wa uhusiano wa chama hicho, Abdul Kambaya amesema katazo la Mahakama limewataja watu watatu akiwemo Profesa Lipumba na Magdalena Sakaya.

"Katazo limewataja watu watatu, mkutano mkuu unaitishwa na Baraza Kuu, wao watakuja kama waalikwa tu," amesema Kambaya.

Muda mfupi, baada ya RPC wa Ilala kuondoka, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba aliingia katika eneo la mkutano na kupokelewa kwa shangwe huku akiingizwa kwenye ukumbi ambao waandishi wa habari wamezuiwa kuingia.

Awali, Kambaya amesema mkutano rasmi unatarajiwa kufunguliwa Machi 14, 2019 akisema leo na kesho kutakuwa na mambo ya kiutawala.



Chanzo: mwananchi.co.tz