Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waweka kambi eneo la mkutano wa ACT Wazalendo

48966 Polisispic

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Takribani askari polisi 20 wametanda nje ya ukumbi wa PR wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ulipokuwa ufanyike mkutano wa ndani wa ACT-Wazalendo.

Mkutano huo uliokuwa ufanyike kuanzia leo asubuhi Jumatano Machi 27, 2019 umezuiwa na polisi huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akisema wameuzuia baada ya kupokea taarifa za viashiria vya vurugu.

Mwananchi ambalo limepiga kambi nje ya uwanja huo limeshuhudia gari lenye maji ya kuwasha likiondoka eneo hilo na kubaki gari ndogo tatu zikiwa na askari wenye silaha.

Tangu leo asubuhi askari hao wamekuwa wakimzuia kila aliyekuwa akiingia katika ukumbi huo.

Kadri muda unavyokwenda magari ya polisi katika eneo hilo yanazidi kupungua, hadi saa 5:02 asubuhi yalikuwa yamebaki matatu, huku askari watano wakiwa wamesimama katika mlango wa kuingia katika ukumbi huo, kumuuliza maswali kila aliyesogelea mlango huo.

"Wewe na abiria wako potea kabla hatujaamua kutoa upepo wa pikipiki yako,” amesikika akisema askari mmoja, akimueleza dereva pikipiki aliyekuwa amempakia abiria.

Akizungumza na Mwananchi katibu wa ACT, Dorothy Temu amesema kuwa hawakupewa taarifa yoyote kuhusu zuio la mkutano huo.

"Hatujaonywa, kilichotokea ni kwamba polisi waliweka kambi tangu asubuhi na kila mwanachama aliyefika eneo hilo alifukuzwa na waliokuja kwa makundi walitawanywa" amesema Temu.

Viongozi wakuu wa ACT leo saa 7 mchana watazungumza na waandishi wa habari kuhusu zuio hilo la polisi.

Polisi wazuia mkutano wa ndani wa ACT-Wazalendo



Chanzo: mwananchi.co.tz