Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waruhusu kongamano CUF kwa masharti

79219 Pic+kongamano

Wed, 9 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Jeshi la polisi Mkoa wa Tabora limeruhusu kongamano la Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na ufunguzi wa matawi ya chama hicho katika Wilaya ya Tabora kwa sharti la kutokuwa na shamrashamra.

Jana Jumanne Oktoba 8, 2019 Kamanda wa polisi Wilaya ya Tabora, George Bagyemu alikiandikia barua chama hicho kuzuia kongamano na ufunguzi wa matawi  wilayani humo, shughuli zilizopangwa kufanyika leo na kesho.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa ziara ya mwenyekiti wa chama hicho,  Profesa Ibrahim Lipumba ya kukiimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 24, 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na Lipumba leo Jumatano Oktoba 9, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,  Barnabas Mwakalukwa ameruhusu kufanyika kwa kongamano na ufunguzi wa matawi bila shamrashamra.

Amesema kutokana na hofu ya Mungu na mamlaka aliyopewa na wananchi kazi anayofanya inazingatia weledi.

"Usifanyike mkutano usiokuwa halali kama mtafungua tawi nakufanya shamrashamra ni mkutano na maofisa wangu watakuwepo kuwachukulia hatua.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
"Kama mtafungua tawi mkatembea kwenda kufungua tawi lingine huo ni mkutano mimi sitakuwepo ila wapo mtakaokutana nao huko,” amesema Mwakalukwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz