Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

...Polisi wapiga waandishi wa habari wakimkamata

97621 MBOWE+AACHIWA+PIC ...Polisi wapiga waandishi wa habari wakimkamata

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro akiwamo wa gazeti la Mwananchi, Janeth Joseph walijikuta katika wakati mgumu katika mkutano wa Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe baada ya askari polisi waliovaa sare na wengine kiraia kuwapiga kwa vitako vya bunduki walizokuwa wabeba.

Kabla ya kutokea vurugu hizo, juzi katika mkutano wa Mbowe uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya Nkoromu katika Kata ya Masama kati wilayani Hai, polisi walivamia gari la mbunge huyo wakitaka kuingia ndani kwa nguvu, ndipo mwandishi huyo aliyekuwa katika majukumu yake ya kazi akipiga picha alinyang’anywa simu na kisha wakaanza kumpiga.

Mwandishi mwingine aliyeshambuliwa na askari hao ni wa Global TV, Elia Peter.

Akizungumzia tukio hilo jana, Janeth alisema kabla ya kuanza kuchukua matukio katika mkutano huo alijitambusha kwa askari hao kuwa yeye ni mwandishi, hivyo akataka ushirikiano na askari hao.

‘’Tulipofika eneo la mkutano tulijitambulisha kwa askari waliokuwa eneo la viwanja vya Nkoromu kwamba sisi ni waandishi wa habari, nashaanga nikiwa nachukua matukio wakati Mbowe anazingirwa na askari hao, mmoja wao ambaye nimemtambua sura alinifuata akaninyanganya simu yangu’’

“Nilipomuuliza ni kwanini amechukua simu yangu wakati nilijitambulisha kwao kuwa mimi ni mwandishi wa habari, alivua silaha yake aliyokuwa amebeba na kuanza kunishambulia sehemu za kifuani.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Nilipata maumivu makali kifuani. Nilifika Kituo cha Polisi Boman’gombe kwa ajili ya kupata PF3 ili niende kupatiwa matibabu. Baada ya kupata matibabu nilirudi kituo cha polisi kutaka kufungua RB, nilinyimwa mpaka RPC wa Kilimanjaro, Salum Hamduni alipoingilia kati,” alisema Janeth.

Kamanda Hamduni aliagiza jalada lifunguliwe kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo dhidi ya askari huyo wa kituo cha Polisi Bomang’ombe.

“Taarifa za tukio hilo nimezisikia, nimemwagiza mwandishi akachukuliwe maelezo yake, ili lifunguliwe jalada la uchunguzi,’’ alisema Kamanda Hamduni.

Chanzo: mwananchi.co.tz