Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi walivyozuia msafara wa CHADEMA Morogoro

Chadema Pichhhhhhhhhh Polisi walivyozuia msafara wa CHADEMA Morogoro

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa viongozi wa Chadema umezuiliwa na polisi mjini Morogoro wakati wakielekea kwenye mkutano wa ndani ulioandaliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini, Devotha Minja.

Mkutano huo uliwakutanisha mawakala wa Chadema kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya usajili wa wanachama kielektroniki na mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.

Akizungumzia mkasa huo uliotokea jana Oktoba 16, 2022, Ofisa wa Chadema Kanda ya Pwani, Gervas Lyenda ambaye alikuwepo kwenye msafara huo, amesema msafara wao ulizuiliwa na polisi katika eneo la Nanenane.

Amesema wanachama wa Chadema walikwenda kumpokea Mnyika mitaa ya Nanenane lakini polisi walizuia msafara huo na kuwataka kupita njia ya vichochoroni badala ya barabara kuu waliyokuwa wakiitumia.

“Tulipouliza kwanini wakasema hapo mbele kwenye hoteli ya Morena kuna mkutano wa viongozi. Mnyika akahoji kama kuna mkutano, kwanini mmezuia magari ya Chadema pekee wakati mengine bado yanapita, wakasema ni maelekezo kutoka juu,” amesema Lyenda.

Amesema walibishana kwa nusu saa, ndipo akafika kiongozi mmoja wa polisi ambaye aliwaruhusu kupita na kuendelea na safari yao.

“Tuliendelea na msafara wetu na sasa tuko kwenye mkutano kama ulivyopangwa,” amesema ofisa huyo wa Chadema.

Jitihada za kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu hazikufanikiwa, hata hivyo zuio hilo liliondolewa muda mfupi baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live