Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wadaiwa kumsaka Lema hotelini, wamkosa

99340 Lema+pic Polisi wadaiwa kumsaka Lema hotelini, wamkosa

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu wanaodhaniwa kuwa Polisi leo Jumanne Machine 17 wamefika katika hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema lakini hawakumpata. Meneja mkuu wa hoteli hiyo, Venance Mkisi amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa polisi hao waliokuwa wamevaa kiraia walifika asubuhi hotelini hapo na kumuulizia Lema. "Ni kweli kwamba Lema alilala hapa na ni mteja wetu wa muda mrefu. Lakini leo aliondoka mapema sana na ameondoka bila kuaga wala kulipa. Hakurudisha ufunguo reception," amesema Mkisi. "Nimefika hapa asubuhi naambiwa kulikuwa na sekeseke, polisi waliokuwa wamevaa kiraia walifika na kumuulizia, lakini waliambiwa kuwa hayupo. Walifuata utaratibu wakaenda na mtu chumbani kwake lakini hawakumpata," ameongeza Mkisi. Meneja huyo amesema hawana wasiwasi naye kwani ni mteja wao wa siku nyingi ambaye hajawahi kuwaletea shida. Taarifa za kufuatiliwa kwa Lema na Polisi zilisambaa mitandaoni tangu asubuhi, ambapo ukurasa wa Chadema Tanzania ulieleza tukio hilo. Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kimondoni, Mussa Taibu alipoulizwa kwa simu alisema hana taarifa. Naye Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa kwa simu alisema yuko kwenye kikao. Lema alitarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari leo, lakini mkutano huo uliahirishwa asubuhi.

Chanzo: mwananchi.co.tz