Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polepole atoa neno sakata la machinga

Polepole Polepole atoa neno sakata la machinga

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Humphery Polepole, ameishauri serikali kuwa makini katika kutatua suala Machinga ili kuepusha vurugu na mchafuko wa amani katika taifa.

Ametoa kauli hii wakati akiwa katika darasa lake la mtandaoni, na kusema ni vyema kuzingatia uchambuzi wa wadau kuhusu uhakika wa soko katika maeneo ambayo watahamishiwa machinga hao.

“Kuhusu habari ya wamachinga tuwe ‘very carefully’ (makini) na hii ‘issue’ (suala) kwa sababu ukikurupuka tu na hii issue inakwenda vibaya lazima tu ‘apply’ sayansi kwenye jambo hili kwa nini watu wapo barabarani kwa mfano usiwahamishe mpaka wamekujibu kwanini wapo barabarani, hapa nazungumzia uchambuzi wa wadau,”

“Halafu waulize eti nikikutengenezea soko mahali fulani utakwenda au huendi atakupa sababu za kwenda atakupa kwa maana ya zile nzuri na mbaya halafu wewe utaangalia je inawezekana kumpeleka kule sasa kwa mazingira ya sasa hivi,” amesema Polepole.

Wiki iliyopita Rais Samia Suluhu akiwaapisha mawaziri Ikulu, jijini Dodoma aliagiza wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuwapanga vyema na kuonya anayoyaona kwenye runinga ya ngumi, kupigana, kufukuzana, kuchafuliana na vitu kumwagwa, hataki kuyaona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live