Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polepole atangaza CCM kusimamia matibabu ya Wasanii waliopata ajali

1.jpeg Polepole atangaza CCM kusimamia matibabu ya Wasanii waliopata ajali

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kinafuatilia kwa ukaribu na kuhakikisha wasanii watatu ambao ni Luludiva, Belle9 na Bonge la Nyau ambao wamepata ajali hii leo wakati wakitokea mkoani Iringa wanapata matibabu haraka.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika.

“Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka” Polepole

LIVE: KUTOKA CHALINZE LULU DIVA, BELLE 9 NA BONGE LA NYAU WAPATA AJALI CHALINZE

Chanzo: millardayo.com