Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polepole ashusha ujumbe mzito kuelekea Mkutano Mkuu CCM

Polepole Ashusha Ujumbe Mzito Kuelekea Mkutano Mkuu CCM Polepole ashusha ujumbe mzito kuelekea Mkutano Mkuu CCM

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwatakiwa mkutano mwema wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM huku akieleza jambo aliloona ni la tofauti kwa desturi ya chama hicho.

Ujumbe huo umesomeka hivi:

"Kwa wana CCM wenzangu na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Nawatakia Mkutano Mkuu Mwema.

Nimeona vipeperushi vyenye picha za Makada wa Chama chetu wakiwaalika wajumbe wa Mkutano Mkuu Dodoma na kuwapongeza kwa kuchaguliwa.

Desturi moja ninaijua kwa hakika, anayealika Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni mtu mmoja tu naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye anauitisha Mkutano Mkuu. Mtu mwingine kuchukua jukumu hilo kwa utashi wake mwenyewe kuwaalika wajumbe inaweza kutafsirika vinginevyo na kinyume na desturi nzuri na misingi ya Maadili ya Chama chetu.

Kama wanaoalika wanachama wana maslahi na Mkutano Mkuu wa CCM kwa maana ya kuomba dhamana ya Uongozi hasa Ujumbe wa Halmashauri Mkuu ya CCM Taifa basi watakuwa wamekosea sana, watakuwa wamemkosea Mwenyekiti wa CCM na wanajaribu kujionesha kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kinyume na desturi na Maadili ya Chama chetu.

Imeandikwa kwenye Katiba ya Chama chetu “Nitasema kweli Daima na fitina Kwangu Mwiko”, nikiona makada wasio na dhamana ya kusema kwa niaba ya Mwenyekiti kwa jukumu la kuwaalika wajumbe wa Mkutano Mkuu nitapenda kutumia uhuru wangu kusema na kulinda Kiti na kubaki katika rekodi kwamba nimeliona hilo haliko sawa na ikajulikane hivyo.

Nawaombea kwa Mungu wajumbe wa Mkutano Mkuu mnapokwenda kutekeleza Jukumu lenu, mkafanye hivyo kwa uaminifu, uadilifu na kwa maslahi mapana ya Chama chetu na Nchi yetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live