Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polepole asema Waitara ameanza ‘kudamshi’

15860 Pic+polepole TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema uamuzi alioufanya Mwita Waitara kutoka Chadema na kuhamia CCM umemfanya aanze ‘kudamshi’ (kupendeza).

Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 5, 2018, katika mkutano wa kampeni za ubunge wa kumnadi Waitara katika kampeni za ubunge wa Ukonga zilizofanyika kata ya Mzimuni.

Awali, Polepole alimsimamisha Waitara huku akiuliza wananchi 'Kadamshi hajadamshi' ambapo wananchi walijibu kwa kusema 'Kadamshi' huku wakishangilia.

Polepole amewataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua Waitara ili apeleke mawazo yao serikalini kwa kuwa atakuwa huru kuongea na kila kiongozi.

"Mkichagua upande wa pili imekula kwenu kwa sababu, hawatoki hata kuongea na CCM sasa mnafikiri watawawakilisha vipi maendeleo ataleta lini wakati amefungwa mdomo," amesema.

Amesema alipita maeneo mbalimbali kuangalia jimbo hilo na amebaini changamoto mbalimbali ambazo sasa Serikali kupitia ilani ya CCM ndiyo itakayotatua.

Polepole amesema kwa sasa chama chake kimefanya mapinduzi makubwa na kuongeza siku hizi mwana CCM unapita mtaani macho makubwa hakuna anayewasumbua

"Siku hizi CCM hakuna figisu kila kitu kitakwenda sawa Waitara alikimbizwa na figisu huko,” amesema Polepole.

Amesema miaka ya nyuma mambo yote yalikuwa yanakwenda polepole kama jina lake "Lakini sasa tumepata jembe ambalo linakimbiza, kwa miaka miwili ameweza kufanya mambo yaliyokwama kwa miaka 20.”

"Kuna mambo mbalimbali ikiwemo treni ya umeme, sasa hivi tuna reli ya kimataifa inaendelea kujengwa na sasa inakaribia huko Morogoro,” ameongeza.

Polepole amesema, "Lakini watu wanasema hakuna tunachokifanya mimi nawaangalia tu na kucheka. Treni ikikamilika mtaiona kwanza ikifika Dar sehemu yake ya kusimama ni ghorofani imetengwa sehemu yenye urefu wa ghorofa tatu ya nyumba.".

Akiendelea kumwaga sera, Polepole amesema, "Treni hiyo ikikamilika itarahisisha biashara zenu ambazo zinachelewa kwa ajili ya foleni, lakini watu wanasema hakuna tunachokifanya."

Polepole  amewataka wananchi hao kupiga kura kwa wingi akisema "tarehe 16 mkapige kura kama zote na mjitokeze kwa wingi kama wote."

Chanzo: mwananchi.co.tz