Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polepole, Slaa na Gwajima kikaangoni

Polepolee Pic Data Polepole, Slaa na Gwajima kikaangoni

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeazimia kuwaita wabunge watatu wa chama hicho iki kuwapa nafasi ya kuwasikiliza baada ya kujadili taarifa za mwenendo wao.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 17 na wa halmashauri kuu ya CCM taifa itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka ilieleza kuwa wabunge hao walioazimiwa kuitwa ni Jerrry Slaa (Mbunge wa Ukonga), Josephat Gwajima (Mbunge wa Kawe) na Hamphrey Polepole (Mbunge wa kuteuliwa).

Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania Samia Suluhu imekutana leo, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Aidha taarifa ya Shaka haikusema wabunge hao ni lini watasikilizwa lakini inasema kuwa hatua ya kuwaita viongozi hiyo inatokana na kanuni za uongozi na maadili toleo la mwaka 2017 na katiba ya CCM ya mwaka 1977, toleo la 2020.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz