Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pofesa Baregu afariki Dunia, wanasiasa wamlilia

PROFESA BAREGU Pofesa Baregu afariki Dunia, wanasiasa wamlilia

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwanazuoni maarufu Prof. Mwesiga Baregu ambaye pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Submitted by Elbogast on Jumapili , 13th Jun , 2021 Prof. Mwesiga Baregu, enzi za Uhai wake.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha  amesema, Prof. Baregu amefariki dunia saa tano usiku wa kuamkia leo akiwa ICU (chumba cha uangalizi maalum)  na alikuwa hapo kwa takribani siku 15.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itikadi na Uhusiano wa Kimataifa wa Chadema, John Mrema amesema chama kitatoa taarifa rasmi taarifa baada ya kikao na wanafamilia kwani ndio wanaelekea hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wakati wa uhai wake Profesa Baregu licha ya kuwa mhadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini pia alitumikia nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema na mlezi wa vijana wa chama hicho.

Katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wamemuelezea mwananzuoni huyo kama muasisi wa kuendesha siasa za kisayansi ambazo si za mikikimikiki ya majukwaani huku akiwa na kauli zenye upeo mpana kwa kumfanya kila mmoja aweze kutafakari.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameandika; "Msiba wa Prof. Mwesiga Baregu ni mzito sana. Hakika mchango wake mkubwa katika ujenzi wa demokrasia ya nchi yetu na haswa katika mchakato wa Katiba ambayo yeye alikuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba utakumbukwa Daima. Alikuwa Mwanazuoni wa Umma na Mhadhiri mahiri”.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara,  Profesa Kitila Mkumbo ameandika "Pumzika kwa amani Profesa Baregu. Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao”.

Chanzo: eatv.tv