Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pingamizi na rufaa 15,380 zawasilishwa kwa wasimamizi

Pingamizi na rufaa 15,380 zawasilishwa kwa wasimamizi

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

odoma. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Selemani Jafo amesema  hadi zoezi la maamuzi ya rufaa lilipokamilishwa jana (Novemba 9 2019) jumla ya rufaa 4, 921 (sawa na asilimia 32) zilipitishwa na zilizobakia zilikosa sifa.

Akizungumza leo Jumapili Novemba 10 2019, Jafo amesema jumla ya pingamizi na rufaa mbalimbali zipatazo 15,380 ziliwasilishwa.

Amesema kazi yote ya kuchukua na kurejesha fomu ilikuwa na changamoto kwa wagombea wengi kufanya makosa mengi ya kikanuni yaliyosababisha wengi wao kutoteuliwa.

“Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na kujidhamini wenyewe, kutojaza fomu namba IV, kutofautiana kwa majina, kutojaza fomu kikamilifu, kuandika umri kimakosa (mfano amezaliwa mwaka 2019) na makosa mengine mbalimbali,” amesema.

Amesema hali hiyo inatokana na baadhi ya vyama kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kuwaelekeza wanachama wao.

Chanzo: mwananchi.co.tz