Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pinda aunda mkakati kumng’oa Msigwa Iringa Mjini

35136 PIC+PINDA Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda

Mon, 7 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewataka wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kuhakikisha katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, mgombea wa chama hicho tawala anashinda ubunge wa Iringa Mjini.

Mbunge wa Iringa Mjini ni Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema aliyeibuka na ushindi mwaka 2010 na 2015.

Pinda ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 6, 2019 katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho mkoani Iringa uliokwenda sambamba na kumchagua mwenyekiti mpya wa CCM mkoani humo.

Amesema kwa sasa ni muda muafaka kwa wanachama wa chama hicho kujitathmini makosa gani huwa wanayafanya wakati wa uchaguzi mpaka jimbo hilo kwenda upinzani.

“Tunahitaji kufanya uchunguzi kwa nini jimbo lipo upinzani. 2020 ni muhimu likarudi CCM tu, nataka kujua, je ni wapiga kura ndio tatizo au wana CCM wenyewe tunashindwa kusimamisha mgombea tunayemtaka,” amehoji Pinda.

Amesema ni muhimu kujua wanachama wangapi wanajiandikisha na wangapi hawajitokezi kupiga kura.

“Uchaguzi huu najipanga vizuri nataka kuzungumza na wanachama wa CCM kata kwa kata, mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji nijue changamoto zao kuhakikisha tunarekebisha makosa na kulikomboa jimbo,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz