Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pinda: Makundi yanaiumiza CCM

98317 Pic+pinda Pinda: Makundi yanaiumiza CCM

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda amewaasa wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kuchagua kiongozi asiye na makundi kwani yamekuwa yakikimaliza chama hicho.

Pinda ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Machi 7, 2020 wakati akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Dodoma Mjini.

Amesema makundi siku zote yanakimaliza CCM na kuwagawa wanachama jambo alilosema linawagharimu kwa kiasi kikubwa wanachama.

CCM Dodoma kinafanya uchaguzi huo ikiwa imepita miezi miwili tangu alipotimukiwa madarakani mwenyekiti wake Robert Muwinje katika sababu ambazo zinatajwa ni kukiuka kanuni.

"Tunapozungumzia suala la usafi ni vigumu sana kumpata mtu wa aina hiyo, lakini msichague mtoa rushwa na kikubwa zaidi msilete mtu mwenye kugawa makundi maana hiyo ndiyo mbaya zaidi," amesema Pinda.

Mjumbe huyo amewataka wana CCM kumchagua mtu ambaye yuko tayari kwa ajili ya kukifia chama na mwenye kujitoa zaidi kwa ajili ya chama chake kwa wakati huu.

Pia Soma

Advertisement
Wajumbe 996 wamehudhuria mkutano huo kati ya 1400 waliotakiwa kuhudhuria kutoka kata 41 na viongozi wa ngazi za juu wanaoishi ndani ya wilaya hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz