Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peneza ampongeza OCD kwa kuzuia sherehe zao za wanawake

45852 Peneza+pic Peneza ampongeza OCD kwa kuzuia sherehe zao za wanawake

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Upendo Peneza amempongeza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita (OCD) kwa kuzuia sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani iliyokuwa imeandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

Sherehe hizo zilikuwa zimepangwa kufanyika jana Ijumaa katika ukumbi wa Moyo wa Huruma uliopo mjini Geita ambapo mgeni rasmi alikuwa awe, Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee.

Hata hivyo, Polisi wilayani humo mkoa wa Geita walizuia sherehe hizo kupitia barua iliyotolewa na mkuu wa polisi wilaya (OCD), Ally Kitumbu iliyotolewa juzi Alhamisi Machi 7, 2019.

Katia barua hiyo kwenda kwa katibu wa Chadema, Geita yenye kumbukumbu namba GE/B.3/24/VOL.V11/63 iliwataka wanawake kushiriki maadhimisho hayo maeneo ya Bugulula halmashauri ya wilaya na viwanja vya soko jipya yanakoadhimishwa na halmashauri ya mji.

Baada ya kuzuia, wanawake wa Chadema wakiwa wamevalia sare zao walikwenda katika viwanja vya Bugulula ambako kulikuwa na watu mbalimbali wakiwamo wanawake wa CCM ambao nao walikuwa wamevalia sare za chama hicho.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Peneza ambaye ni mbunge kutokea mkoa wa Geita alimshukuru OCD huyo kwa kuzuia sherehe yao kwani imempa fursa ya kuzungumza na wanawake.

“Namshukuru sana OCD, kwani sababu kama si yeye nisingepata fursa ya kuongea na akina mama zangu wa CCM, Chadema na wananchi kwa ujumla namna hii,” alisema Peneza.

“Niseme tu OCD, Mungu akitubariki akatufikisha tarehe nane mwezi wa tatu mwaka ujao sisi hatutakaa tuandae tena sherehe za akina mama, tutashirikiana na Serikali tunafika hapa,” aliongeza huku akishangiliwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz