Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pazia uchaguzi ACT-Wazalendo lafunguliwa

93328 Pic+act Pazia uchaguzi ACT-Wazalendo lafunguliwa

Tue, 28 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha ACT -Wazalendo nchini Tanzania kimefungua pazia kwa wanachama wake wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua fomu.

Nafasi zitakazogombewa ngazi ya Taifa ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi, mwenyekiti wa Taifa, makamu mwenyekiti Taifa - Tanzania Bara na Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa halmashuri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane)

Akizungumzia na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 27, 2020 katibu mkuu wa chama hicho,  Dorothy Semu amesema uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika Machi 14, 2020 ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee, ngome ya vijana na ngome ya wanawake.

Amesema nafasi zitakazowaniwa katika ngome ya wanawake ni mwenyekiti wa ngome, makamu mwenyekiti wa ngome, katibu, wajumbe wa halmashauri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi 8).

Katika ngome ya vijana, nafasi ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti - Tanzania Bara na Zanzibar, katibu na naibu wake, wajumbe wa halmashauri kuu na mkutano mkuu Taifa.

Amesema nafasi zinazowaniwa katika ngome ya wazee ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti Tanzania Bara na Zanzibar, katibu na naibu wake, wajumbe wa halmashauri kuu Taifa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Pia Soma

Advertisement
"Januari 27 mpaka Februari 26 ni muda wa kuchukua fomu,  Machi 7 ni uchaguzi ngome ya wazee; Machi 8 ni uchaguzi ngome ya vijana, Machi 9 ni uchaguzi ngome ya wanawake na Machi 14 itakuwa ni uchaguzi wa chama," amesema katibu mkuu huyo.

Semu amesema fomu hizo zinapatikana na kurejeshwa ofisi ya makao makuu Kijitonyama, ofisi kuu ya Vuga Zanzibar, ofisi za ACT Wazalendo mikoa yote.

Chanzo: mwananchi.co.tz