Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambalu aahidi kujenga ofisi mpya Kanda ya Victoria

John Pambalu Sef John Pambalu.

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), John Pambalu ambae ametia nia ya kugombea Uenyekiti wa Kanda ya Victoria katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho amesema iwapo atateuliwa kugombea nafasi hiyo mojawapo ya kipaumbele chake ni kujenga ofisi mpya katika kanda hiyo.

Akizungumza nasi, Pambalu amesema ofisi zilizopo kwa sasa ni za kukodi na haziendani na hadhi ya chama hicho kwa kanda ya Victoria hivyo kuwapo haja ya kujengwa ofisi mpya jambo ambalo amesema ataanza nalo.

“Nitaifanya Kanda ya Victoria kuwa ngome ya kisiasa na kwa utajiri wa watu ilionao inastahili kuwa na ofisi yake na siyo za kukodi kama ilivyo sasa, inastahili ofisi ya kisasa ambayo itatoa taswira na picha pana ya watu ambao wapo tayari kuleta mageuzi” amesema Pambalu.

Katika kanda hiyo kwa nafasi ya Uenyekiti, Pambalu anachuana na Mbunge wa zamani wa Nyamagana ambaye ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Ezekiel Wenje.

Kamati Kuu ya chama hicho ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe imemaliza usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za kanda na kichachosubiriwa ni kutangazwa kwa waliopenya katika mchujo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live