Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

POLEPOLE:BARABARA ZA JUU KUJENGWA ZAIDI

5ebf65804617b989ae389dae77450aaa POLEPOLE:BARABARA ZA JUU KUJENGWA ZAIDI

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka huu, chama hicho kinatarajia kujenga barabara za juu katika jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya mataa ya Chang’ombe, Morocco, Mwenge, Magomeni, Fire,Tabata, makutano ya barabara ya Umoja wa Mataifa, Ali Hassan Mwinyi na Kinondoni.

Polepole amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita katika ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa maendeleo ya watu yanakwenda na vitu ndiyo maana ilani hiyo imejikita kuboresha miundombinu mbalimbali na kubeba mambo mengi zaidi tofauti na ile ya mwaka 2015.

Katika hatua nyingine Polepole aliwahimiza wananchi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam kuudhuria mkutano wa kampeni ya mgombe urais kwa tiketi ya CCM Rais John Magufuli, mkutano unaotegemewa kufanyika hapo kesho kuanzia saa moja kamili asubuhi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, unaotarajiwa kuanza saa moja kamili asubuhi hapo kesho.

Chanzo: habarileo.co.tz