Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Olenasha ataka wananchi kumchagua Kalanga Monduli

17540 KALANGA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Naibu Waziri wa Elimu William Olenasha  amesema kama wakazi wa Jimbo la Monduli wanataka maendeleo wanatakiwa kumchagua mgombea ubunge wa CCM,  Julius Kalanga.

Olenasha ambaye pia ni meneja kampeni za jimbo hilo ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 15, 2018 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu.

Amesema Monduli wanapaswa wachague maendeleo, si kulinda sifa au heshima ya mtu binafsi.

“Maendeleo yanapatikana kwa kuunga mkono chama kilichopo madarakani kinachosimamia Serikali na sio vinginevyo,"amesema.

Amesema 2015 watu wa Monduli walipishana na gari ya mshahara kwa kuchagua upinzani.

"Kwa miaka mitatu sasa Rais wetu John Magufuli  kaelekeza nguvu za maendeleo vijijini na kuna mabadiliko makubwa katika sekta zote,” amesema.

Amesema Monduli imekuwa nyuma kwa sababu Chadema haitoi ushirikiano kwa serikali.

"Nafasi imejitokeza ya kusahihisha makosa, msirudie makosa fanyeni chaguo sahihi, Kalanga wa CCM," amesema.

Amesema ushindi wa CCM katika jimbo hilo ni dhahiri kwani wamefanya kampeni za kistaarabu na za maendeleo.

"Kampeni zetu hazikuwa na matusi wala vitisho, tumefika kwa wananchi kusikiliza kero zao na baadhi kutatuliwa papo kwa papo," amesema.

Kwa upande wake Kalanga ameomba kura ili awe mbunge na kuweza kutatua kero za wananchi wa Monduli.

"Mimi ni kijana wenu kama mlivyoniamini mwaka 2015 naomba mniamini tena kwani safari hii nipo na Serikali ambayo sote tunaona inafanya kazi nzuri," amesema.

Amesema atazifanyia kazi ahadi zote ikiwamo tatizo la maji, migogoro ya ardhi na shida ya umeme.

Chanzo: mwananchi.co.tz