Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ole Sendeka alitaka Bunge liache kulalamika, lichukue maamuzi

OLE SENDEKA 222 Ole Sendeka

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olesendeka, amelitaka Bunge liache kulalamika kwa maamuzi yake iliyokwisha fanya, badala yake litoe maazimio ya kuwachukulia hatua watu wanaoshindwa kufanyia kazi maazimio yake.

Ole Sendeka ametoa ushauri huo jana Jumatano, tarehe 8 Februari 2023, bungeni jijini Dodoma, akichangia hoja zilizowasilishwa na kamati za kudumu za mhimili huo.

Ametoa kauli hiyo wakati akinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyoandika katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, yaliyosema viongozi kukubali kufanywa vikaragosi ni dalili ya woga na si dalili ya heshima.

Ole Sendekea aliendelea kunukuu maneno ya Mwalimu Nyerere akisema, mwaasisi huyo wa Tanzania aliandika kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta , viongozi halisi hawapendi kuishiriki na kwamba kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya uoga na kukaribisha udikteta.

“Nayatumia maneno haya sababu sifurahii kuona Bunge likilalamika juu ya maamuzi ambayo mmekwisha fanya, ningependa tutoke na maazimio kwamba wale walioagizwa wayafanye tuwajue ni kina nani, wanapaswa kusimamia katika sekta hizo na Bunge lielezwe nani hawa wanaokaidi,” amesema Ole Sendeka na kuongeza:

“Sisi tuko hapa kwa niaba ya wananchi, tuchukue hatua kama hatuna mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya waziri mmoja mmoja, dhidi ya mtendaji mmoja mmoja, tuchukue hatua hata kwa wale ambao tuna mamlaka nao ili wawasimamie hawa ambao wamepewa dhamana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live