Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ogopa sana sub za dakika za majeruhi - Ally Hapi

Hapi WA0007 Ogopa sana sub za dakika za majeruhi - Ally Hapi

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Umoja wa VWazazi CCM, Ally Salum Hapi amesema atashirikiana na wenzake kufanya kazi usiku na mchana kuijenga Jumuiya mpya ya Wazazi akisema mara nyingi Kocha (Rais Dkt. Samia) anapofanya sub dakika za mejeruhi (kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu) anakuwa na mahesabu yake hivyo yupo tayari kwa mapambano na amewataka Wapinzani wasitegemee huruma kwakuwa muda wa huruma umekwisha.

"Comrade Issa amesema mahala ambapo kuna gari ambalo injini inahitaji msaada huwezi kupeleka baiskeli ikavute niwaahidi Jumuiya ya Wazazi tutakwenda kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunajenga Jumuiya mpya ya Wazazi ambayo itasadifu sura na uzuri wa Chama chetu, kwahiyo Ndugu zangu wa Jumuiya nyingine wajipange Baba kama alikuwa usingizi ameamka, kazi inaendelea"

Akiongea Jijini Dar es salaam leo Aprili 05,2024 wakati wa mapokezi ya Sekretarieti, Hapi amesema "Tunayo kazi mwaka huu 2024 na mwakani 2025 ya kukiletea ushindi Chama chetu na Mimi nipo tayari kushirikiana na wenzangu na Viongozi wetu kuhakikisha, kwasababu unajua sisi Wachezaji tunaoingia dakika za majeruhi kwenye sub.

"Dkt. Samia ni kama Kocha sasa anapopanga kikosi cha kwanza kinaweka msingi baadaye akaangalia akaona mchezo huu unahitaji kiungo wa kutoa mpira akamleta Dkt. Nchimbi, akaona lazima tufanye super sub tuingize Viungo wengine, Washambuliaji wengine, sasa ogopa sana sub ya dakika za majeruhi mara nyingi Kocha anakuwa na mahesabu yake"

"Niwahakikishie Wana CCM wenzangu tupo tayari kwa mapambano na wale Jamaa wa upande wa pili ambao kazi yao ni kelele tu, Rais amewatengenezea mazingira mazuri, wanafanya mikutano, wanafanya shughuli zao, wamepewa ruzuku lakini shukrani hawana, niliwasikia wengine wanalalamika kwenye Uchaguzi mdogo wanasema mbona hawajatuachia alaah! yaani CCM iwaachie Kata kweli?, wasitegemee huruma"

"Muda huruma umekwisha, habari ya kubebwa hakuna twende kwa Wananchi tukarejeshe heshima ya Chama chetu, uchungu wa Mwana aujuae Mzazi, nani kama Wazazi?, nani kama Dkt. Samia?"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live